Kigamboni Kwa Yesu ni ufunuo wa miaka saba (2024-2031) ambao Mungu alimpa mtumishi wake Kamanda Dr. Peter Bujari Octoba 17, 2019. Aliandika ujumbe huo kwa mara ya kwanza kwenye ukurasa wake wa face book Octoba, 18, 2019 kuwa “Kigamboni itakuwa ufalme wa Mwanakondoo akirejea kitabu cha Zakaria 4:6. Mwaka 2024 Juni, alirudishiwa maono wakati wa mkutano wa Injili kuwa afanye maandalizi na wakati ulikuwa umefika. Wakati huu aliambiwa kuwa uamsho unalenga kuleta miaka saba (2024-2031) ya neema na ustawi wa watu wa Kigamboni. Aliambiwa kuwa kuna madhabahu za shetani na maagano ya shetani juu ya ardhi ambayo yanapaswa kuvunjwa ili kuruhusu neema ya Mungu kuwa juu ya watu. Kwa ajili ya maagano hayo, kuna vitu vikubwa haviwezi kufanyika Kigamboni.
Nchi ambayo imejaa neem ana ustawi ambayo watu wake wanamtegemea Mungu (Jehova) na kumwamini mwanae Yesu Kristu
Kushirikisha madhehebu yote ya Kigamboni yanayoendana na kuamini katika maono ya Kigamboni Kwa Yesu kuziharibu kazi za shetani (1John 3:8) na kuruhusu mapenzi ya Mungu kutawala.
Namna ya kufikia maono: Maono haya yatafikiwa kwa:
Wanufaika: Wanufaika wa uamsho huu ni watu wote wakaao Kigamboni, waingiao na kutoka kwenye malango ya Kigamboni. Litatimia lile neno la kumbukumbu 28:6 utabarikiwa uingiapo na utokapo.
Nani wajiunge: Watu wote wanaotaka kuwa sehemu ya mabadiliko ya kiroho, kuruhusu ufalme wa MUNGU kutawala Kigamboni. Wanaochukia ibada za shetani na miungu mingine
Namna ya kujiunga: Unaweza kujiunga kwa whats up HAPA. Au wasiliana nasi kwa barua pepe: kigambonikwayesu@peterbujari.com au kwa simu: 0658 536 110
KAMATI YA KIGAMBONI
KWA YESU INAWAKARIBISHA KATIKA MKUTANO MKUBWA WA INJILI
TAREHE 06-10 NOVEMBER, 2024 I UWANJA WA KIMBUNGA, MJIMWEMA